Skip to content

Karibu tukuhudumie, furaha yetu ni kukuhudumia

MATAMANIO YETU

Kupanua wigo wa wanachama kwa kuwahamasisha wafanyakazi wa Benki Kuu matawi mengine kujiunga na chama chetu. Lengo kubwa ni kuongeza Mtaji wa taasisi ili kufikia matarajio ya wanachama ya kuinua hali za maisha yao kupitia huduma zitolewazo na chama hasa mikopo.

Chama kinatarajia kuongeza idaid ya watumishi ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wanachama. Kutoa mafunzo kwa wanachama hasa elimu ya ushirika na ujasiliamali inayolenga kuongeza tija kwa shughuli zao, Kutoa elimu kwa viongozi wa chama na watendaji ili kuongeza ufanisi wa kazi na kuendeana na mabadiliko ya uchumi na technolojia.

Kuanzisha miradi mbalimbali itakayosaidia kuongeza mapato ya chama.

Mikopo

Mkopo wa Maendeleo

Kiwango hadi TZS 50,000,000/=
Muda wa marejesho ni miezi 36
Riba ni 8% ya jumla ya mkopo wote

Mkopo wa Dharula

Kiwango hadi TZS 5,000,000/=
Muda wa marejesho ni miezi 6
Riba ni 8% ya jumla ya mkopo wote

Mkopo wa BOTFASTER

Kiwango hadi TZS 1,000,000/=
Muda wa marejesho ni miezi 2
Riba ni 10% ya jumla ya mkopo wote

“Kuwa Saccos ya mfano, yenye utoshelevu wa rasilimali fedha kwa ajili ya kuwahudumia wanachama wake na jamii kwa ujumla”

– MAONO YA SACCOS YETU.

Back To Top